KICHUYA AAHIDI MABAO ZAIDI TAIFA STARS... asema anataka afunge na atoe pasi nzuri za mabao

BAADA ya kuanza vizuri michuano ya Cosafa kwa kupachika mabao mawili, Shiza Kichuya amesema anataka mabao zaidi.

Akihojiwa nchini Afrika Kusini, Kichuya alisema angependa kufunga mabao zaidi kutokana na nafasi zinavyopatikana.

“Mimi ni mchezaji ambaye ningependa kupata nafasi zaidi ya timu ya taifa kufunga mabao zaidi, tutajengea imani zaidi kwa kocha, lakini nitakuwa naisaidia timu.”

“Kweli napenda kufunga zaidi, ikishindikana kabisa nitoe pasi nzuri niisaidie timu kucheza vizuri au kupata mabao,” alisema.


Kichuya alifunga mabao mawili katika mechi ya kwanza ya Taifa Stars wakati ilipoitwanga Malawi kwa mabao 2-0 na yeye kuibuka shujaa mwisho wa mchezo huo.

No comments