Habari

KIINGILIO CHA PAMBANO LA MAYWEATHER, MCGREGOR AGOSTI 26 NI MIL 21

on

PAMBANO la bingwa wa ngumi za
uzito wa juu, Floyd Mayweather na mpinzani wake, Conor McGregor, linatarajiwa
kufanyika Agosti 26 na waandaaji wa pambano hilo wametangaza kiingilio cha juu
ni dola 10,000, zaidi ya Sh milioni 21.
Mbali na kuwawekea kiasi hicho
cha juu, wametangaza kiasi cha chini kwamba kitakuwa cha dola 500 sawa na sh
1,096,300. Kiingilio hicho cha chini kitawafanya watazamaji kukaa kwenye jukwaa
la juu mbali kidogo na eneo la ngumi.
Bei hiyo ya tiketi inaonekana
kuwa kubwa dhidi ya ile ya pambano la Mayweather na Manny Pacquiao
lililofanyika Mei 2015, huku kiingilio cha juu kikiwa dola 7,500, zaidi ya
milioni 16 na kiasi cha chini kikiwa dola 1,500, zaidi ya milioni 3,288,900.
Pambano hilo la kihistoria
linatarajiwa kuteka hisia za mashabiki wengi kutokana na mpinzani wa
Mayweather, McGregor kuwa na uwezo wa hali ya juu.
Pambano hilo litafanyika kwenye
ukumbi wa T-Mobile Arena, uliopo Las Vegas na tiketi hizo zimeanza kuuzwa jana
nchini Uingereza.
Mayweather na McGregor wameanza
kutambiana kuelekea pambano hilo, huku McGregor akisema kwamba atahakikisha
kwenye raundi ya nne anamaliza pambano hilo kwa kumchapa KO.
“Sitakuwa na muda wa kupoteza,
ninaujua uwezo wa mpinzani wangu, hivyo lengo langu ni kuhakikisha ninalimaliza
katika raundi ya nne kwa kumpiga KO,” alisema McGregor.
Mwishoni mwa wiki iliyopita
bingwa Anthony Joshua, alitembelea kwenye mazoezi ya Mayweather na kumpa mbinu
za kumpiga mpinzani wake. Joshua ameweka wazi kuwa Mayweather ana nafasi kubwa
ya kuwa bingwa kutokana na uwezo wake.

“Sina wasiwasi na Mayweather
kutokana na uwezo wake, niweke wazi kuwa mimi ni shabiki wa timu ya Mayweather
TMT, hauwezi kuongea lolote juu ya staa huyo, nina imani kubwa ubingwa lazima
achukue, nimeanza kumjua Mayweather tangu nikiwa na umri mdogo na mara zote
amefanya makubwa,” alisema Joshua.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *