KITAMBI CHA BEENIE MAN CHAZUA GUMZO MITANDAONI

RAPA wa miondoko ya Dance Hall, Beenie Man raia wa Jamaica amegeuka gumzo kwenye mitandao ya kijamii kufuatia picha aliyoposti kwenye mitandao akionekana kunenepa na kuota kitambi.

Staa huyo kwa kawaida ni mwembamba na mwenye mwili mkavu lakini hivi sasa ameanza kunenepa na kuota kitambi, hali iliyoanza kuathiri mwonekano wa umbo lake.

Beenie Man aliwahi kutamba na kibao cha “Welcome the King of Dance Hall” amekuwa kimya kwa muda mrefu na kushangaza watu alipoibuka akiwa amefuga tumbo.


“Ni Beenie Man ninaemjua au nani,” ilisomeka moja kati ya posti zilizotumwa baada ya picha kuonekana.

No comments