KIUNGO WA MBEYA CITY ANAYESUBIRIWA KUTUA YANGA AFICHUA KUNYATIWA NA SIMBA

KIUNGO mpya anayesubiriwa kutua Yanga, Raphael Daudi amefichua mipango ya Simba kutaka kumsajili akisema amewaambia watulie na kwamba atakapohama Mbeya City sasa kutua kwake ni Yanga tu.

Habari zilizopatikana zinasema kuwa Daudi ambaye kwa sasa yuko katika kikosi cha taifa Stars amesema Simba SC wamekuwa wakimfuata mara baada ya kurudi kutoka Afrika Kusini lakini amewaambia kwa sasa anataka kwenda Yanga.

Daudi amesema ameamua kuichagua Yanga kutokana na kubaini kwamba ndiyo sehemu sahihi kwake katika kwenda kuendeleza kupaji chake na pia heshima waliyompa mapema kwa kuzungumza naye kwa umakini.

Kiungo huyo ambaye alifanya makubwa katika mashindano ya COSAFA na kupiga penati ya mwisho ilitoihakikishia Stars ushindi wa tatu katika mashindano hayo, tayari Yanga wameshamalizana na Mbeya City kwa kulipia uhamisho huo akibaki mwenyewe kusaini.

“Simba kweli wamenifuata wananitaka niungane nao lakini suala hilo nimewaambia kwa sasa litakuwa gumu kwasababu nipo hatua za mwisho kumalizana na Yanga,” alisema Daudi.

“Yanga nimeona ndiyo sehemu sahihi kwangu kwa sasa sitaki kwenda sehemu halafu nikaenda kuua kipaji changu lakini hapohapo tayari Yanga wameshamalizana na Mbeya City kwa kulipa fedha za uhamisho kwa kuwa bado nilikuwa na mkataba wa mwaka mmoja nilichobakiza ni kusaini tu na zoezi hilo limetokana na kwamba sasa nipo katika timu ya taifa."

No comments