KLABU YA SUNDELAND YASEMA KIFO CHA BRADLEY LOWERY NI MSIBA MZITO KWAO

KLABU ya Sunderland ya Uingereza imesema kwamba kifo cha shabiki wake mkubwa mtoto wa umri wa miaka sita, Bradley Lowery ni msiba mkubwa kwa klabu hiyo.

Mtoto huyo ambaye tatizo lake la kiafya liligusa nyoyo za watu wengi amefariki dunia juzi Ijumaa na klabu hiyo imesema kwamba msiba huo ni wa mashabiki wote wanachama na mashabiki na wanatazama namna gani watafanya jambo la kumuenzi.

Lowery alikuwa anaugua ugonjwa ambao wa kwa Kiingereza hufaamika kama “Neuroblastoma” na unatajwa kuwa ni aina ya saratani adimu sana na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo tangu akiwa na umri wa miezi 18.

Lowery alifanywa kuwa kibanzo ama nembo ya klabu hiyo na akaunda urafiki wa ukaribu na mchezaji wa klabu hiyo Jrmain Defoe.

Aidha aliwaongoza wachezaji Waengland kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.

No comments