KLOPP ADHAMIRIA KUMALIZA JUU ZAIDI YA NAFASI YA NNE MSIMU HUU

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza kkikosi chake kitakuwa na nguvu zaidi mwaka huu na amedhamiria kumaliza juu zaidi ya nafasi ya nne waliyoishia msimu uliopita.

Klopp alipoungana na vijana wake Daniel Sturridge, Sadio Mane, Jordan Henderson, Roberto Firmino na James Milner ambao walikuwa ni baadhi ya wachezaji walioripoti kwenye uwanja wa mazoezi wa Melwood kwa ajili ya kuchekiwa kama wako fiti kuanza mechi za kirafiki.

“Sote tunafahamu kuwa wiki chache zijazo tutatakiwa kucheza mechi za kufuzu UEFA na lazima kuwe na presha,” Klopp aliuambia mtandao wa Liverpoolfc.com.

“Lakini tuna muda mzuri wa kujiandaa, muhimu tuendeleze pale tulipoishia msimu uliopita. Sote tunajua lolote ninaweza kutokea.”

“Tunafahamu pia tuko Top 4 England, hivyo tunafanya kila jitihada kuwa bora zaidi.”


“Kikosi kitakuwa imara zaidi mwaka huu. Ndio maana tuna imani mazuri yatatokea msimu ujao,” aliongeza.      

No comments