Habari

KOCHA LWANDAMINA AKATISHA FUNGATE LA YONDANI… amtaka kusahau raha za mke mpya na kuelekeza akili dimbani

on

BEKI kisiki wa klabu ya Yanga, Kelvin Yondani, amerejeshwa kikosini haraka na kocha Geogre Lwandamina
ambaye ameanza kukisuka upya kikosi hicho kabla ya kufunguliwa kwa msimu mpya wa
Ligi.
Yondani ndio kwanza ametoka
kwenye fungate baada ya kufunga ndoa na mkewe lakini amelazimika kukatisha
mapunziko yake kwasababu ya kuwahi program za kocha.
“Yondani tayari ameripoti baada
ya kumaliza shughuli zake za harusi na tumempokea tukiamini anajifua ili
kupigania namba kwenye kikosi cha kwanza msimu ujao,” amesema Lwandamina.
Lwandamina amesema, amemkaribisha beki huyo na kumwambia anatakiwa kusahau raha za
nyumbani na kuhamishia mawazo yake uwanjani ili kuisaidia Yanga iweze kufanya
vizuri.
Amesema anafahamu kuwa Yondani
ni beki mzuri mwenye uwezo mkubwa na alikuwa na mchango mkubwa kwenye ubingwa
wa msimu uliopita hivyo bado ana imani naye kuwa anaweza kufanya vizuri na
kuisaidia timu hiyo kufikia malengo.

Yondani ametimiza msimu wa nne
tangu atue Yanga akitokea Simba na ameweza kuipa mafanikio makubwa timu hiyo
ikiwemo mataji matatu ya Ligi ya Vodacom na Kombe la FA.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *