KOCHA LWANDAMINA AMKABIDHI DONALD NGOMA JUKUMU LA "KUIMALIZA" SIMBA

KUFUATIA upinzani mkali uliopo kwa timu za watani wa jadi hapa nchini, kocha wa klabu ya Yanga, George Lwandamina raia wa Zambia amekabidhi jukumu la kuimaliza Simba kwa Donald Ngoma ambaye aliongeza miaka miwili ya kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Ligi Kuu bara.

Lwandamina amesema kuwa anafahamu namna ambavyo mchezaji huyo anahofiwa na wapinzani wake kutokana na usumbufu wake kwa mabeki na soka lake la matumizi makubwa ya nguvu.

“Unapoona mchezaji anatajwa sana na vyombo vya habari wakati wa usajili ujue ana kitu cha ziada ukilinganisha na wengine, imekuwa jambo zuri kumalizana na Ngoma kwa sababu alikuwa kwenye mpango wa klabu kwa muda mrefu,” alisema kocha huyo.

“Nafahamu namna anavyohofiwa na wapinzani, najua ubora wake na hata namna nitakavyomtumia kwa msimu ujao katika nafasi ya ushambuliaji,” alisema.


Donald Ngoma alikuwa akihusishwa kutaka kutua Simba lakini kumbe ilikuwa janja ya nyani kwani tayari mshambuliaji huyo alikuwa amemaliza masuala yake muhimu na Yanga kwa muda mrefu.

No comments