KOCHA OMOG ATAKA MANYIKA PETER ASISEPE SIMBA SC

WAKATI baba wa golikipa wa Simba, Manyika Peter akitaka mwanawe huyo aruhusiwe kuondoka katika klabu ya Simba, kocha wa wekundu hao hataki kulisikia hilo.

Peter Manyika ambaye amewahi kuwa kipa wa timu ya Tanzania na yanga, amekuwa akilalamika kwamba mwanawe amekuwa akipigwa benchi Simba na hivyo anataka aondoke kwenda kujaribu kucheza mahala.

Hata hivyo, saluti5 inafahamu kuwa kipa huyo nambari mbili yuko katika mipango ya kocha Joseph Omog na kocha huyo amesema kwamba hataki Manyika aondoke.


Omog amedaiwa kupingana na hoja ya kumuondoa Manyika akisema anamtegemea sana katika kikosi chake.

No comments