Habari

KOCHA POCHETTINO AUKUBALI “MSULI” WA VICTOR WANYAMA

on

POCHETTINO wa Tottenham ni kama
vile huwezi kumwambia kitu chochote juu ya kiwango cha kiungo raia wa Kenya,
Victor Wanyama.
Hii ni baada ya kocha huyo
kukiri kuwa katika usajili ujao wa majira ya kiangazi hafikirii kabisa kuigusa
idara ya kiungo kutokana na uwezo wa “jembe” hilo la maana.
Akinukuliwa na BBC, kocha huyo
alisema mchezaji huyo ana sifa, nguvu na uwezo wa kuisaidia sana klabu hiyo.
“Ni mnyama, ninamfahamu vyema
kwa sababu nilimnunua nikiwa Southampton kutoka Celtic. Ni rahisi sana kutambua
sifa hizi,” alisema.
Meneja huyo alikuwa anajibu
maswali kuhusu umuhimu wa mchezaji huyo kwa klabu hiyo kwenye kikao na
wanahabari katika kituo cha mafunzo cha klabu hiyo London.
Pochettino raia wa Argentina
alijiunga na Spurs Mei, 2014 kwa mkataba wa miaka mitano na Mei mwaka huu
aliongeza mkataba huo na kuahidi kusalia White Hart Lane hadi 2021.

Wanyama alitua Spurs kwa dau la
pauni mil 11 akitokea Southampton katika dirisha la mwezi Juni, mwaka huu.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *