KOCHA SLAVEN BALIC ASEMA MARKO ARNAUTOVIC ATAWAFAA MSIMU UJAO

KUNA makocha wachache sana duniani wenye pumzi ya kumsifu mchezaji mmoja mmoja katika kundi la wachezaji wengi.

Lakini kwa upande wake kocha wa Westham United, Slaven Bilic anaamini kwamba baada ya uhakika wa kumpata Marko Arnautovic, jembe hilo litawafaa sana katika msimu ujao wa Ligi.

Arnatovic aling’ara sana katika Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga na sasa anahamishia makali yake katika kikosi cha wapiga nyundo hao.

Bilic amesema kwamba nyota huyo raia wa Australia atakuwa kama shoka ambalo lilikuwa linasubiriwa kukaka msimu mkubwa.

“Arnautovic atakuwa mtu wa kutusaidia sana. Ni mchezaji mwenye vitu vingi sana uwanjani na anajua wapi anatakiwa kukaa na kusaidia wenzake,” amesema.

“Marko alikuwa katika kikosi cha Inter Milan na Werder Bremen sio kwa sababu alikuwa anacheza tu bali kwa sababu alikuwa na kipaji kikubwa,” ameongeza.

Kocha huyo amesema kwamba anataka kusuka kikosi kikali sana msimu huu na kwamba hana mashaka na wachezaji wapya wanaoingia katika timu yake.


“Kila mchezaji anayeingia anakuja kwa sababu ya mapendekezo maalum. Ni wakati wa kusuka Westham mpya.”

No comments