KOCHA WA PSG AKUNWA NA USHINDI WAO DHIDI YA MONACO

KOCHA wa timu ya Paris Saint-Germain,  Unai Emery amesema kwamba amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na timu yake Jumamosi, baada ya kutoka nyuma na kishwa wakaondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya  Monaco katika mchezo wa  Trophee des Champions.

Katika mchezo huo PSG  walikuwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Mabingwa hao wa Ligue 1  hadi  timu hizo zinakwenda mapumziko, lakini cha pili wakaweza kuzinduka na kuweza kutwaa taji hilo la Trophee des Champions  kwa mara  ya tano mfululizo wakishukuru mabao yaliyowekwa kimiani na nyota wao, Dani Alves  na  Adrien Rabiot.

Kikosi hicho cha Djibril Sidibe ndicho kilikuwa cha kwanza kupata bao kipindi hicho cha kwanza, lakini  PSG  wakachomoa  dakika ya sita kipindi cha pili kupitia kwa beki wao huyo wa zamani wa  Juventus,  Dani Alves kabla ya staa huyo kumpigia pande  Rabiot  dakika 12 baadae.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mechi hiyo  Emery alisema kwamba  alichokishuhudia ni mbili nzuri kutoka kila upande  na zote zina wachezaji wenye vipaji ndani na hata nje ya uwanja.

 "Tuliudhibiti mchezo na tulikuwa wazuri kwenye  safu ya ushambuliaji licha ya wao kuwa wabaya kwa kufanya mashambulizi ya kushutukiza . Lakini pia na sisi tulitengeneza nafasi nyingi za hatari,”alisema kocha huyo.

"Tulichokuwa tunakita ni kuendelea kusakata soka letu na timu ilionyesha jinsi wanavyoweza kutulia na hilo ndilo jambo la muhimu,”aliongeza kocha huyo.

No comments