Habari

KUMBAKIZA SANCHEZ ARSENAL NI SAWA NA NGAMIA KUPENYA TUNDU LA SINDANO

on

ALEXIS SANCHEZ anataka alipwe pauni 400,000 kwa wiki ili aendelee kubaki Arsenal, vinginevyo anatimka.
Mshambuliaji Alexandre Lacazette aliyekamilisha usajili wa kujiunga na Arsenal jana jioni akitokea Lyon, atalipwa pauni 150,000 kwa wiki.
Sanchez ambaye hadi sasa amegoma kusaini mkataba mpya Emirates huku akiwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, tayari amekataa ofa ya klabu hiyo ya mshahara wa pauni 275,000 kwa wiki.
Manchester City inatajwa kuwa ipo katika hatua nzuri ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Chile, ingawa kocha Arsene Wenger amekuwa akisisitiza kuwa Arsenal haitauza silaha zake kwa wapinzani wake wa Premier League.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *