KURT ZOUMA AJIHAKIKISHIA KUBAKI CHELSEA

BEKI wa kati asie na nafasi Chelsea, Kurt Zouma ametamba kubaki ndani ya klabu hiyo licha ya mabingwa hao wa EPL kuwa na mpango wa kusajili beki mpya wa kati.

Kauli hiyo ni kama inakinzana na hali halisi kuwa Mfaransa huyo anatakiwa kupata nafasi ya uhakika ya kucheza katika mwaka wa Kombe la Dunia na klabu ya Marseille ni mojawapo ya timu za Ulaya zinazomtaka na huenda zikampa nafasi ya kutosha ya kucheza.

Hata hivyo, beki huyo ambaye msimu uliopita alicheza mechi chache za mwisho baada ya kupona jeraha lake la goto lililomweka nje ya dimba kwa takriban mwaka mmoja, amesema wazi kuwa “tutabanana hapahapa.”


“Nina furaha sana hapa Chelsea. Tetesi ninazozisikia zinanipa faraja kuona ninahitajika, ila lengo langu ni kubaki hapa na kuisaidia timu msimu ujao, hivyo jukumu langu ni kujituma tu,” alisema.

No comments