KWA KAULI HII, SANCHEZ HATAKI TENA KUBAKI ARSENAL


Alexis Sanchez amezidi kumtia hofu kocha wa Arsenal, Arsene Wenger  kwa kuweka wazi matamanio yake ya kucheza Champions League.

Mshambuliaji huyo wa Chile amesema njozi yake ni kucheza Champions League (Ligi ya Mabingwa Ulaya), kitu ambacho Arsenal hawatakuwa nacho msimu ujao baada ya kumaliza ligi kuu ya England nje ya top four.

Hiyo inazidi kuzitia mshawasha Manchester City na Bayern Munich ambazo zinawania saini ya Sanchez mwenye umri wa miaka 28.

Sanchez amesema: "Uamuzi sio wangu peke yangu, lakini mimi nimeshafanya maamuzi yangu. Kwasasa nasubiri Arsenal waniambie wanataka nini".

Alipoulizwa ni nini anachokitaka yeye, Sanchez akasema: "Kucheza Champions League na kulitwaa taji. Ni njozi yangu niliyokuwa nayo tangu utotoni. 

"Ila kwa sasa mimi bado ni mchezaji wa Arsenal, mkataba wangu unaisha msimu ujao".No comments