LACAZETTE HANA MSAADA WA KUMBAKISHA ARSENAL ALEXIS SANCHEZ

WAKATI Arsene Wenger alikuwa akiamini ujio wa Alexandre Lacazette utamshawishi Alexis Sanchez kubaki Arsenal, lakini kocha huyo sasa ameanza kuwa na mashaka ya kubaki na mshambuliaji huyo.

Mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki anaoutaka Sanchez ili asaini mkataba mpya, haukubaliki Arsenal na sasa juu yao kuamua kusuka au kunyoa – kumuuza au kumbakisha ili aondoke bure kiangazi kijacho.

Manchester City, Bayern Munich na Chelsea zote zimeonyesha nia ya kutaka saini ya Sanchez kiangazi hiki iwapo atashindwa kuafikiana na Wenger juu ya masilahi yake kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Emirates.

Hata hivyo, Arsenal haina mpango wa kumuuza staa huyo wa miaka 28 kwa timu pinzani katika Premier League na sasa ni wazi kuwa inakabiliwa na hatari ya kumpoteza bila malipo kiangazi kijacho kama watashindwa kufikia makubaliano.

Madai hayo ya Sanchez yanaweza kuwa kikwazo kwa harakati za Wenger kumbakisha Emirates, kutokana na Mfaransa huyo kutokuwa tayari kulipa mshahara huo, badala yake akiamini pauni 275,000 kwa wiki ni kiasi kinachotosha.

No comments