LEICESTER CITY WAMTANGAZIA OFA MLINZI WA HULL CITY

MABINGWA wa zamani wa England, Leceister City wameweka dau mezani kwa ajili ya kumwania mlinzi kisiki wa klabu ya Hull City, Harry Maguire.

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 24 amemalizana msimu uliopita katika kiwango cha kuzivutia timu mbalimbali za Premier.

Lakini, Leceister City ndiyo walioongoza mbio za usajili huo na wameweka mezani ofa ya pauni mil 17 kwa ajili ya kumnasa katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Bosi wa mabingwa hao wa msimu wa mwaka 2016/17, Craig Shakespeare amethibitisha taarifa za kumwinda Maguire na anapambana kwa ajili ya kukamilika kwa dili hilo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

“Klabu inahitaji huduma ya mlinzi huyo mapema iwezekanavyo ili kuimalisha ukuta wa timu hiyo ambayo imetetereka msimu uliopita.”

“Ninakaribia kukamilisha mazungumzo na naamini nitafanikiwa katika kutimiza  hatua hii muhimu kwa ajili ya Leceister City” alinukuliwa  Shakespeare aliliambia gazeti moja.


Harry Maguire ambaye ni mzaliwa wa jiji la Sheffield alijiunga na Hurry City mnamo mwaka 2014 kwa dau la pauni mil 2.5

No comments