LEICESTER CITY YAICHOMOLEA AS ROMA OFA YA KUMTAKA RIYAD MAHREZ

OFA ya klabu ya AS Roma Italia kwenda Leicester City kwa ajili ya kumchukua mshambuliaji Riyad Mahrez imekataliwa.

Kocha Craig Shakespeare amesema kwamba hakuna mchezaji mwenye thamani ndogo katika klabu yake kama ambavyo miamba hao wa Italia wanataka kuonyesha.

Mshambuliaji huyo raia wa Algeria anataka kuondoka katika kikosi hicho baada ya kuwapa mafanikio Leicester na kuwasaidia kutwaa taji la ubingwa la EPL msimu wa 2015/16.

Ingawa haijatajwa kwamba Roma wanataka kutoa kiasi gani lakini habari zinasema kwamba Leicester City wamegoma kumruhusu mchezaji huyo kutokana na kile walichosema kwamba ni kiwango kidogo cha pesa. 

Mahrez mwenye umri wa miaka 26 yuko Hong Kong katika maandalizi ya Ligi Kuu lakini pia wakishiriki michuano maalum ya Kombe la Asia.

Shakespeare ameiambia Sky Sport kwamba anadhani kwamba hakuna mchezaji mwenye bei ndogo kwenye timu yake.

“Nadhani nilikaliliwa kwenye kikao cha mwisho na waandishi wa habari kwamba ofa ya Roma imekataliwa kwasababu hawajafikia malengo yetu. Naomba nishikilie msimamo huo,” amesema.

“Nilikuwa naongea kwa upole zaidi na sasa nasisitiza hilo kwa upole zaidi kwamba waongeze pesa,”amesema kocha huyo.


Roma wamekuwa wakihaha kutafuta mtu mbadala wa kuongeza makali kwenye idara ya  ushambuliaji baada ya kuondoka kwa Mohamed Salah aliyejiunga Liverpool.

No comments