LEICESTER CITY YAPIGANIA KUMBAKIZA VARDY KIKOSINI

KLABU ya Leicester City inapambana kiume kwa ajili ya kutaka kumbakiza straika wake mahiri Jamie Vardy ambaye kwa sasa anawaniwa na timu mbalimbali barani Ulaya.

Taarifa za ndani ya mabingwa hao wa msimu wa mwaka 2016/17 zinasema kuwa uongozi umeketi na Vardy kwa ajili ya kumuongezea mkataba mpya.

Hata hivyo, Vardy mwenyewe bado hajaamua kama anaweza kubaki katika viunga vya “mbweha” hao wa jiji la Leicester. Awali, Vardy alikuwa anaendelea na mazungumzo na bosi wa Leicester City wakati huu ambapo tetesi za usajili zinamuhusisha kujiunga na ama PSG au Juventus.

Akizungumzia kandarasi hiyo mpya, Vardy alisema kwa sasa suala lililo mbele yake sio idadi ya miaka ya kubaki katika klabu hiyo bali ni kukamilika kwa ndoto za kutaka kumbakiza.

Bosi wa “The Fox”, Craig Shakespeare amenukuliwa akisema anamweka Vardy katika malengo yake ya muda mrefu licha ya kutakiwa na timu kadhaa za Ulaya.

“Ninapambana kikamilifu kumbakiza kikosini JamieVardy licha ya ukweli kuwa anatakiwa na klabu nyingi Ulaya.”

“Ni mchezaji muhimu wa kuwa nae ndani ya mkataba mrefu, ninaamini nitafanikiwa ila kuna kazi ya ziada ya kumshawishi,” alisema Shakespeare.

No comments