LEICESTER YATANGAZA DAU LA PAUNI MIL 22 KWA AJILI YA WILLIAM CARVALHO WA URENO

MABINGWA wa England mwaka 2015/16, Leicester City sasa wapo tayari kuweka mezani kitita cha pauni mil 22 kwa ajili ya kumnasa kiungo William Carvalho katika usajili huu unaondelea.

Kiungo huyo raia wa Ureno ameingia katika rada "mbweha"   hao wanaotaka kurejea katika chati ya timu zinazofanya vyema katika premier msimu unaotarajia kuanza mwezi Agosti mwaka huu.

Dalili za kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 kutua katika kikosi cha Leicester City zinatiwa nguvu na taarifa kutoka kwa bosi wa timu ya soka ya Sporting, Marco Silva aliyethibitisha kuweko kwa uwezekano wa kumruhusu Carvalho kuondoka.

Marco Silva amesema Carvalho anaweza kuondoka mwezi huu wa Julai kama kuna klabu inaweza kuweka dau nono mezani.

Wakitambua hilo, Mbweha hao wamemtengea kiungo huyo kitita cha pauni mil 22 wakiongeza dau waliloliweka awali ambalo lilikuwa pauni mil 20. 

Sporting walimthaminisha Carvalho kuwa ni wa dau la mil 35 ingawa ameonyesha dalili za kukubali kushusha kiwango.


No comments