LEWIS HAMILTON ASEMA ATAHAKIKISHA ANAPAMBANA KUBEBA TAJI LA HUNGARIAN GRAND PRIX

MKALI wa mbio za magari wa kampuni ya Mercedes raia wa England, Lewis Hamilton, amesema atahakikisha anabeba taji la Hungarian Grand Prix, ili kurudisha heshima yake.

Hungarian Grand Prix inafanyika leo katika mji mkuu wa Hungary, Budapest, na ni mashindano yanayotarajiwa kuvuta hisia za watu wengi, kutokana na vita ya maneno ya muda mrefu ya madereva wa makampuni ya Mercedes, Ferari pamoja na Red Bull.

Hamilton amesema kuwa, ana hamu kubwa ya kubeba taji hilo pamoja na kuvunja rekodi ya kuongoza kwa kushinda mashindano, akiwa na pointi nyingi kama alivyowahi kufanya Schumacher.

Mjerumani huyo, ambaye aliweka rekodi ya kushinda kwa pointi 68, anaamini atapita na kuandika rekodi yake.

Dereva huyo, licha ya kujipa matumaini, pia anatarajia kupata upinzani wa hali ya juu kutoka kwa hasimu wake wa muda mrefu wa kampuni ya Ferari, Sebastian Vettel, ambaye katika mashindano yaliyopita alimsababishia ajali ambayo ilisababisha ashindwe kuendelea na mashindano.

No comments