LICHA YA OFA MBILI KUKATALIWA, ARSENE WENGER BADO AKOMAA NA THOMAS LEMAR WA MONACO


ARSENE WENGER amekiri kuwa Arsenal ina dhamira ya kutaka kumsajili kiungo wa Monaco, Thomas Lemar, ambaye klabu yake imemthaminisha kwa pauni milioni 80.

Arsenal tayari imekataliwa ofa zake mara mbili – pauni milioni 30 na nyingine ya pauni milioni 40 kwa staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye miaka 21, lakini inatarajiwa kujaribu tena bahati kwa kuweka mezani ofa nyingine.

Wenger, 67, amekataa kufafanua kuhusu uhamisho wa staa huyo, lakini amekiri kuwa hana kizuizi juu ya kufanya usajili mwingine baada ya kuwanasa Sead Kolasinac na Alexandre Lacazette.

No comments