LIONEL MESSI KUZEEKEA BARCELONA …mshahara wake ni ‘kufuru’


YAMETIMIA. Staa wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi, amekubali kusaini mkataba mpya utakaomuweka Nou Camp hadi mwaka 2021, akivuta mshahara unaoelezwa kuwa pauni 500,000 kwa wiki, huku kukiwa na kipengele cha kumruhusu kuondoka kwa dau la pauni milioni 264.

Messi, 30, aliyefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Antonella Roccuzzo nyumbani kwao Argentina wiki iliyopita, amekubali kusaini mkataba mpya na Barcelona mara baada ya kurudi Hispania akitoka fungate huko Antigua na Barbuda na klabu hiyo imethibitisha dili hilo.

No comments