LIVERPOOL SASA YAPANIA KUANGUSHA UKUTA WA SOUTHAMPTON

KAMA unakuwa na beki wako unayemtegemea sana, kisha unaambiwa kuwa beki huyo anaondoka kirahisi sana, utumbo lazima utacheza.

Ndivyo ambavyo viongozi na benchi zima la ufundi la klabu ya Southampton ni kama hawana amani baada ya kuambiwa kwamba Liverpool wameingia kwenye rada zao.

Beki mwenye mapafu ya mbwa wa kikosi hicho, Virgil Van Dijk anatajwa kwamba ameshakamilisha baadhi ya mambo kuhamia kwenye timu ambayo haibahatishi katika usajili, Liverpool.

Na sasa kuna habari kwamba Liverpool kwa miezi kadhaa wamekuwa wakiwania saini ya beki huyo, jambo ambalo linaikosesha amani Southampton.   


Van Dijk ni mmoja wa mabeki wagumu sana katika kikosi hicho na amekuwa muhimili mkubwa katika safu ya ulinzi, hivyo hatua ya Liverpool ni kama kutaka kuuangusha ukuta wake.

No comments