LIVERPOOL YAIAMBIA FC BARCELONA "HATUNA MPANGO WA KUMUUZA COUTINHO"

KATIKA kile kinachoonekana kutaka kuimarika zaidi, klabu ya Liverpool inasema kwa sasa haina mpango wa kumuuza mchezaji wake nyota raia wa Brazil, Philippe Coutinho.

Habari zinasema kwamba klabu ya FC Barcelona ya Hispania ilikuwa imeomba kumsajili mshambuliaji huyo kwa ofa ya kutisha ya pauni mil 72 lakini Liverpool imesema hazitoshi.

Barcelona wanahaha kutaka kumsajili Coutinho wakiwa na wasiwasi kwamba huenda nyota wake mwingine hatari kutoka taifa hilo lenye utajiri wa wanasoka, Neymar akatimkia zake Paris Saint-Germain ya Ufaransa.

Hta hivyo Liverpool imesema kwamba yenyewe iko katika mikakati mikubwa ya kujiimarisha katika michezo ijayo ya Ligi ya mabingwa Ulaya na ingekuwa kituko kama itafanya makosa ya kumwachia nyota wake huyo.

Kocha wa wekundu hao, Jurgen Klopp amesema kwamba klabu yake haina mpango wa kumuuza Coutinho kwa sababu yenyewe ina mikakati ya kujiimarisha zaidi.

“Hatuna mpango wa kumpoteza mchezaji wetu yeyote ambaye tunajua atatusaidia katika msimu ujao. Ndio tunaweza kupata pesa, lakini sio kila wakati pesa inaleta faraja,” amesema Mjerumani huyo.


Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, amepachika mabao 14 na kupika mengine saba katika mechi za mashindano kwenye klabu yake hiyo ya sasa.

No comments