LIVERPOOL YANG'ANG'ANA KUSAKA SAINI YA ALEX CHAMBERLAIN

KLABU ya Liverpool bado inaendelea na jitihada zake za kumsaka mshambuliaji wa Arsenal, Alex Chamberlain ambaye anasuasua kuongeza mkataba kwenye kikosi chake.

Liverpool wanamsaka nyota huyo mwenye kasi ili kumjumuisha na mshambuliaji wao mpya, Mohamed Salah.


Vinara hao wa Anfield wametenga kiasi cha pauni mil 30 ilicha ya kiungo huyo wa Kiingereza kubakiwa na miezi 12 tu kwenye mkataba wake.

No comments