Kocha wa RB Leipzig, Ralph Hasenhuttl ameiambia Liverpool isahau kabisa kuhusu kumsajili Naby Keita.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, anawaniwa kwa udi na uvumba na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, lakini klabu hiyo ya Ujerumani imesisitiza kuwa Keita haondoki kiangazi hiki.

RB Leipzig  imeipiga chini ofa mpya ya Liverpool ya pauni milioni 66.

"Uwezekano wa Keita kujiunga na Liverpool ni sifuri,"alisema kocha wa RB Leipzig.

"Kwa asilimia 100, ni wazi kuwa Naby Keita ataichezea Leipzig msimu huu. Kwetu sisi kila mtu anajua jinsi gani umuhimu wa Keita, hakika atakuwa na RB Leipzig kwenye Champions League".
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac