LIVERPOOL YAZIDI KUTESWA JUU YA USAJILI WA PAUNI MILIONI 60 WA NABY KEITA


Liverpool inaendelea kupewa 'za uso' na klabu ya RB Leipzig juu ya nia yao ya kutaka kumsajili Naby Keita.

Nyota huyo wa kimataifa wa Guinea amekuwa lengo kuu la usajili kwa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, lakini kila ofa aliyopeleka ilipigwa chini na RB Leipzig.

Ofa ya pauni milioni 57 ilikataliwa wiki mbili zilizopita na sasa imeripotiwa pia kuwa ofa mpya ya pauni milioni 66 nayo imekataliwa. No comments