LUKAKU ASEMA WALA HAKUFIKIRIA MARA MBILI KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED


Romelu Lukaku amekiri kuwa hakuhitaji kufikiria mara mbili pale ilipotekea nafasi ya yeye kujiunga na Manchester United.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, anaielezea Manchester United kama klabu kubwa duniani ambayo asingethubutu kuikataa pale walipompa ofa ya kujiunga nayo.

Lukaku amefaulu vipimo vya afya na muda wowote atatangazwa rasmi kama mchezaji mpya wa Manchester United akitokea Everton ambayo nayo imemsajili Wayne Rooney kutoka kwa Mashetani hao wekundu.


No comments