LUKAKU: HUYU MOURINHO HUYU ATANITOA HUYU!

STRAIKA Romelu Lukaku amesema kwamba anavyoamini kocha Jose Mourinho ataweza kulipeleka soka lake katika hatua nyingine.

Straika huyo awali alionekana kukerwa kwa kuuzwa na kocha huyo wakati akiitumika Chelsea lakini sasa anaonekana atakuwa tegemeo kwa Mourinho kutokana na kuwa mmoja wa mastraika ambao anawahitaji Old Trafford.

“Mourinho ni mtu ambaye alinihitaji nicheze chini yake wakati nikiwa na umri wa miaka 10 na sasa nimepata nafasi tena ya kucheza chini yake ni jambo la kujivunia,” staa huyo aliuambia mtandao wa ESPN.

“Tulikuwa tukiwasiliana akinieleza ni jinsi gani klabu inavyonihitaji na ni kitu gani anakitarajia kutoka kwangu,” aliongeza staa huyo.


“Unafahamu tulikuwa pamoja katika kipindi tofauti, kwa ujumla tulikutana nikiwa bado kijana mdogo, nilikuwa na hamu ya kucheza na anafahamu uamuzi wangu wa kuondoka nilikuwa nahitaji kucheza,” aliongeza staa huyo.

No comments