LUKAKU SASA ANUKIA MANCHESTER UNITED KWA PAUNI MIL 100Manchester United inaripotiwa iko mbioni kuipiku Chelsea katika mbio za kupata saini ya mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku kwa dili la pauni milioni 100.

Msimu uliopita, United ilivunja rekodi ya usajili duniani pale ilipomrejesha Old Trafford kiungo Paul Pogba kwa pauni milioni 89, lakini sasa ipo tayari kuandika rekodi mpya kwa Lukaku ambaye anawindwa kwa udi na uvumba na Chelsea.

Lukaku ananukia Old Trafford huku Wayne Rooney aliye mbioni kurejea Everton akiwa chambo cha kulainisha dili la Lukaku.


No comments