MAANDALIZI UZINDUZI WA FILAMU YA "ASALI WA MOYO" YASHIKA KASI

MAANDALIZI ya uzinduzi wa filamu ya ‘Asali wa Moyo’ yanaonekana kupamba moto ambapo wasanii na wadau mbalimbali wa sanaa hiyo wameahidi kuhudhuria.

Uzinduzi huo ambao mgeni rasmi atakuwa mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolela, umepangwa kufanyika Julai 30, mwaka huu ndani ya Mpo Afrika, Tandika Davis Corner, jijini Dar es Salaam. 

Akiongea na ripota wetu, Dar es salaam jana, mwandaaji wa muvi hiyo anayefahamika zaidi kwa jina la Profesa Puto, amesema kuwa tayari madiwani wote wa Wilaya Temeke wamethibitisha kumuunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi.

“Nimepokea pia ahadi ya kuhudhuria kutoka kwa wasanii kadhaa wa bongomuvi ila bado nawaomba wadau, wasanii na mashabiki wengine mbalimbali kujitokeza kwa wingi zaidi siku hiyo ili kushuhudia mapinduzi makubwa ninayokuja nayo katika sekta ya muvi," amesema Puto.

No comments