MABONDIA BONGO WASHAURIWA KUZINGATIA MLO KAMILI

MABONDIA wote nchini wameshauriwa kuhakikisha wanakuwa na afya imara kabla ya kupanda ulingoni kwenye mapambano yao, kwa kuzingatia mlo kamili.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Chama cha Mabondia kilichopewa kibali cha kusimamia mchezo huo nchini, Dk. Donald Madono alipokuwa akiongea na saluti5 ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.

Madono amesema kuwa, mabondia wengi wamejenga utamaduni wa kuamini kuwa, maandalizi katika mchezo huo ni kujifua gym pekee, bila ya kuzingatia kwamba wanatakiwa wawe na afya imara pia.

“Afya nzuri kwa wanamichezo imegawanyika katika sehemu nyingi tofauti, lakini kubwa ni kwenye kuzingatia makundi makubwa matatu ya vyakula ambayo ni wanga, protini na vitamin kwa ajili ya kujiweka sawa,” amesema.


Amesema, afya mgogoro husababisha bondia ashindwe kuwa na ufanisi mzuri ulingoni na kujikuta akiwa na makali yasiyodumu, hata kama atajitahidi kwenye mazoezi.

No comments