TAKRIBAN siku tano tu zimesalia kabla ya ile shoo bab kubwa ya “Usiku wa Kucharuka Kipwani na Singeli” kudondoshwa ndani ya kiwanja cha Dar Live, Mbagala Zakheem, jijini Dar es Salaam Agosti 5, ambapo homa ya mashabiki imezidi kuonekana kuwa kubwa.

Bendi mbili za mipasho za Jahazi Modern Taarab na Zanzibar Stars zitakung’uta burudani ya pamoja katika jukwaa la kiwanja hicho, huku wakali kadhaa wakiwemo Khadija Kopa, Khadija Yussuf, Anifa Maulid, Kivurande Junior na Dullah Makabila wakitajwa kupamba usiku huo.

Homa ya shoo hiyo iliyopangwa kuanza majira ya saa 3:00 usiku na kuendelea hadi majogoo na ambayo kiingilio chake kitakuwa sh. 7,000, imeonekana kuwa kubwa zaidi hasa kutokana na msisimko walionao wapenzi, wadau na wasanii wenyewe ambapo sasa kila mmoja anajinasibu kufunika kwa burudani kali.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac