MAJERUHI YAMBAKISHA MBARAKA YUSUPH AFRIKA KUSINI

STRAIKA wa Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph amebaki Afrika Kusini baada ya kikosi cha Stars kurejea alfajiri ya jana kikitokea nchini humo kilipokwenda kushiriki michuano ya Cosafa.

Mbaraka aliyesajiliwa na klabu ya Azam hivi karibuni kwa msimu ujao wa Ligi Kuu bara, inadaiwa kumgharamia matibabu baada ya kuumia akiwa na Stars.

Akizungumza jana akiwa Afrika Kusini, Mbaraka alisema amebaki nchini humo ili kuendelea na matibabu ili akirejea awe fiti kwa msimu ujao.

“Nimesalia Afrika Kusini kwa matibabu kutokana na majeraha niliyopata na nashukuru Mungu naendelea vizuri na kuanzia Jumatano naweza kuanza kujiandaa kurudi nyumbani.”

Kikosi cha Stars kimerejea nchini baada ya kumaliza nafasi ya tatu michuano hiyo na kujinyakulia kitita cha dola 10,000 sawa na sh. Mil 22 za Kitanzania.


Wachezaji wa kikosi hicho cha Stars wameweka kambi jijini Mwanza kujiandaa na mechi dhidi ya Rwanda ya kuwania kufuzu michuano ya Afrika “Chan” kwa wachezaji wa Ligi ya ndani itakayopigwa Julai 15, mwaka huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

No comments