Habari

MALKIA WA NYUKI AREJEA MSIMBAZI KUONGEZA NGUVU… aahidi kuipeleka Simba kambi nje ya nchi

on

KLABU ya Simba inawakusanya
matajiri wake wote ili kuongezea nguvu katika kipindi hiki cha kuisuka Simba
mpya.
Baada ya viongozi wakuu wa
Simba, Evans Eveva na makamu wake, Geofrey Nyange “Kaburu” kukabiliwa na kesi
ya jinai iliyowasabasbisha kuwekwa rumande hadi Julay 13, mwaka huu, baadhi ya
wafadhili wa zamani wa Simba wamerejea katika kuhakikisha Simba inasonga mbele.
Habari zilizoifikia saluti5
zinasema kwamba mmoja wa matajiri hao ni mfanyabiashara Rahma Al Kharoos maarufu
kama “Malkia wa Nyuki” ambaye miaka minne iliyopita alikuwa akiifadhili Simba
katika mambo mbalimbali.
Mwanamama huyo anayefanya
biashara zake katika nchi ya Asia amedaiwa kuwa anataka kuipeleka Simba katika
kambi ya mwezi mmoja nje ya Tanzania mara baada ya kumalizika kwa zoezi la
usajili.
“Unajua malkia amesema wazi
kwamba baada ya kuona viongozi wana matatizo, yeye amehaidi kuongeza nguvu
lakini mchango wake ni katika kuiweka Simba katika kambi iliyotulia na anataka
wakakae nje ya Tanzania,” kimesema chanzo chetu.
Habari za uhakika zinasema
kwamba mfanyabiashara huyo amejitolea kuiweka Simba katika kamba maalum nchini
Oman kwa mwezi mzima na anataka jambo hili aachiwe yeye.
“Anataka katika kipindi hiki
yeye aigharamie timu kwa mwezi mzima na anataka kuona Simba haiyumbi,” amesema
na kuongeza.

“Bahati njema ni kwamba Simba
kuna watu wengi wana uwezo kila mmoja anataka kuonyesha namna ambavyo klabu na
timu inasonga mbele.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *