MAN CITY: SANCHEZ AKIENDA PSG TUTAKOMAA NA MBAPPE

KLABU ya Manchester City inasemekana itaelekeza nguvu zake zote ili kuhakikisha wanamnasa straika wa AS Monaco, Kylian Mbappe, endapo staa wa Arsenal, Alexis Sanchez, ataamua kwenda kukipiga PSG.


Kwa sasa vinara hao wa Ligi Kuu England wamekuwa wakiisaka kwa udi na uvumba saini ya straika huyo wa Arsenal, lakini inavyoonekana kwa sasa huenda wakamkosa endapo PSG watatangaza dau nono kuliko la kwao.

No comments