MANCHESTER CITY WATAJWA KUMMEZEA MATE STRAIKA ANDRE AYEW WA WESTHAM UNITED

STRAIKA wa Westham United, Andre Ayew anawindwa na matajiri wa jiji la Manchester, Manchester City ingawa kutakuwa na kazi ya ziada kumng’oa.

City imekuwa katika mbio za kumsainisha nyota huyo kwa dau la pauni mil 27.

Hatua ya City kutaka kumwita kundini mtoto huyo wa mfalme wa zamani wa soka barani Afrika, Abed Pele ni kutokana na mkakati wake wa kutaka kusuka kikosi bora cha kumaliza Ligi ya premier kwa mafanikio makubwa.

City iliyoshindwa kutetea taji la premier msimu wa 2015/16, ilimweka katika wakati mgumu kocha Manuel Pellegrini na sasa imepanga kuingia sokoni kusajili nyota kadhaa walio bora.

“Ayew ni kati ya wachezaji muhimu kwa sasa ulimwenguni, ana kipaji cha kuweza katika klabu yoyote kubwa hivyo City haipaswi kumwacha.”

No comments