MANCHESTER UNITED BADO HAIJAACHANA NA FABINHO


MANCHESTER UNITED inaendelea na mazungumzo na kiungo wa Monaco ya Ufaransa, Fabinho, licha ya kuwa inakaribia kumtangaza Nemanja Matic kuwa mchezaji wake mpya akitokea Chelsea.

Tayari United imekubaliana dili na Chelsea kwa ajili ya Matic ambaye Jose Mourinho anamjua vizuri baada ya kutwaa naye taji la Premier League msimu wa 2014/15, lakini kwa mujibu wa gazeti la The Independent, bado Mourinho anataka ingizo jingine ili kuimarisha safu yake ya kiungo.

Dili la Matic la pauni milioni 35 litakamilika mara tu baada ya mbadala wake, Tiemoue Bakayoko wa Monaco kumalizana na Chelsea juu ya masilahi yake kabla kuhamia Stamford Bridge.


Mourinho anaamini Fabinho ambaye hivi karibuni alipiga picha akiwa ameshika jezi ya United, atakuwa bidhaa muhimu msimu ujao, akiwa na uwezo wa kucheza kiungo na beki ya pembeni.

No comments