Habari

MANCHESTER UNITED ISHINDWE YENYEWE KUMSAJILI IVAN PERISIC

on

Kocha wa Inter Milan Luciano Spalletti amesema winga anayewaniwa na Manchester United,  Ivan Perisic anaweza kuondoka kiangazi hiki – lakini ni pale tu watakapopata mbadala wake.
United ambayo tayari imewasajili mshambuliaji Romelu Lukaku kwa pauni milioni 75 na beki Victor Lindelof kwa pauni milioni 30.7, imekuwa ikihusishwa kwa nguvu na usajili wa  Perisic mwenye umri wa miaka 28.
Hata hivyo usajili huo umening’inia hewani baada ya winga huyo kujumuishwa  kwenye kikosi cha Inter katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya huko China na Singapore.
Spalletti  amesema ingawa ni Perisic ni mchezaji wao muhimu lakini kama United itakuja na ofa sahihi, hawatasita kumpiga bei.
Kocha huyo akasema   hilo pia litategemea na suala la kumpata mbadala wake.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *