MANCHESTER UNITED KUMPOKEA IVAN PERISIC WIKI IJAYOMANCHESTER UNITED inaamini kuwa dili la kumtwaa winga Ivan Perisic linalokadiriwa kuwa kati ya pauni milioni 45 na 50 limefikia pazuri na gezti la The Independent limeripoti kwamba staa huyo raia wa Croatia atatua Old Trafford wiki ijayo licha ya klabu yake ya Inter Milan kudhamiria kumbakisha.


Perisic, 28, amefunga mabao 20 katika mechi 79 tangu atue Inter mwaka 2015, lakini kuelekea msimu wa 2017/18 amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa kuhamia Old Trafford, huku akielezwa kuwa tayari amekubaliana na United kuhusu masilahi yake binafsi.

No comments