MATIAS KRANEVITTER AKIRI KUWANIWA NA CHELSEA NA MAN CITY

NYOTA wa klabu ya Atletico Madrid, Matias Kranevitter amekiri tetesi za kuwaniwa na timu kadhaa za premier, lakini Chelsea na Manchester City ndio zinazoongoza mbio hizo.

Lakini Matajiri wa jiji la London, Chelsea wameongeza kasi ya kumwania kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, kwa ajili ya kutua Darajani katika usajili wa majira ya kiangazi.

Awali, Kranevitter amekuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kujiunga na washika mitutu wa jiji la London, Arsenal.

Akinukuliwa, kiungo huyo amesema ndoto zake za kutua Emirates zinaweza kuyeyuka kwa sababu Chelsea wameongeza kasi ya mazungumzo.

“Nimekuwa nikisikia malengo ya Chelsea kwangu na kadri ninavyotambua mpango upo hivyo.”

No comments