MAVUGO AWASHAURI SIMBA KUACHANA NA BEKI WA LYON SPORT YA RWANDA

STRAIKA wa klabu ya Simba raia wa Burundi Laudit Mavugo amewadokeza siri nzito viongozi wa klabu hiyo kwamba waachane na suala la kumfuatilia beki wa Lyon Sport, Manzi Thierry akiamini kuwa nyota huyo ana kiwango cha kawaida tofauti na mabeki wazawa.

Simba ilikuwa na mipango ya kumleta beki huyo kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara pamoja na michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Manzi ambaye yupo katika kikosi cha taifa cha timu ya Rwanda, Amavubi amekuwa katika rada za Simba kwa ajili ya kuinasa saini yake lakini ili kuimarisha safu yao ya ulinzi.

Mara baada ya kujiridhisha na kiwango chake Simba imeamua kuachana na beki huyo na tayari inekuwa ni kama jambo linaloonekana kuwa neema kwa watani wao Yanga ambao wameanza kutupa ndoano kwa mlinzi huyo wa kati.

Yanga tayari imeanza mikakati hiyo baada ya kujiridhisha kwa kiwango alichokionyesha katika mechi kati ya Taifa Stars na Rwanda iliyopingwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mavugo amesema kwamba anamfahamu vizuri Manzi kutokana na kuwahi kukutana nae mara kadhaa wakiwa katika majukumu ya timu zao za taifa hivyo anaamini kwamba beki huyo ana tofauti na mabeki wazawa.

Alisema anamfahamu vizuri kutokana kucheza nae klabu moja nchini mwake na kusema kuwa ni beki mzuri lakini bado anaamini kuna mabeki wazuri zaidi wa hapa nchini waliomzidi kiwango.

“Ni beki mzuri lakini ukiangalia uwezo wake na mabeki wa hapa nchini ninaamini bado Tanzania kuna wenye uwezo mzuri ambao wanamzidi kiwango,”alisema.


Mavugo alisema ana imani na usajili unaofanywa na uongozi wa klabu hiyo kwa kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mechi za msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

No comments