MAWAKALA AFRIKA KUSINI WAWAHAHIA AISHI MANURA, MUZAMIRU YASSIN WA STARS

WAKALA wa kuuza wachezaji wa nchi ya Afrika Kusini wamevutiwa na viwango vya wachezaji wawili kutoka ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" kwa ajili ya kuwauza barani Ulaya.

Wanandanga hao ambao nao pia ni wachezaji wa timu ya Simba ni Muzamiru Yassin na Aishi Manura ambao wakala wa nchini humo wanapigana vikumbo kwa ajili ya kuanza mazungumzo nao.

Kikosi cha Stars kipo nchini Afrika Kusini wakishiriki michuano ya COSAFA kama timu mwalika ambapo katikati ya wiki walikuwa wakimenyana na timu ya taifa ya Zambia katika hatua ya nusu fainali.

Mawakala Mnabole Siwekwa na Mhadtat Mkwanoy ambao wanafuatilia kwa karibu michuano hiyo wameweka bayana azma ya kutaka kuwafafutia timu wanandinga hao wawili.

Taarifa zilizotufikia mwanzoni mwa juma zimesema kuwa wakala hao wamevutiwa na kiwango cha wachezaji hao wa wekundu wa Msimbazi mara baada ya kuwaona katika mechi dhidi ya Malawi na ile dhidi ya Bafanabafana.

Muzamiru anayemudu kucheza katika idara kiungo ametajwa kuwa chaguo la baadhi ya klabu nyingi za daraja la pili chini Afrika Kusini pamoja na zile za barani Ulaya.

Kutokana na kigezo hicho, mawakala hao wamesema wanahaha kutaka kuanzisha mazungumzo baina ya wachezaji hao lakini wanabanwa kutokana na ulinzi uliopo kambini mwa Stars.

Juu ya Aishi Manula, wamakala wamekiri kuvutiwa na uwezo alionesha wa kulinda lango la Stars na kwamba amewekwa katika orodha ya wachezaji waliong’ara katika michuano hiyo ya COSAFA.


Harakati za mawakala hao zimewataja pia wachezaji kama Shiza Kichuya na Abdi Banda ambao pia wameonyesha kiwango cha kucheza soka la kulipwa nje ya mipaka ya Tanzania.

No comments