MAXIME NA KAGERA SUGAR YAKE KUANZA KAMBI YA MAZOEZI JULAI 17

KOCHA wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema baada ya kumaliza mafunzo yake ya ukocha kwa sasa akili yote ameihamishia kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara ambapo amepanga kuanza mazoezi Julai 17, mwaka huu.

Hivi karibuni Mexime alihitimu kozi ya daraja A ya shirikisho la soka Afrika (CAF), iliyofanyika makao makuu ya shilikisho la soka Tanzania (TFF), jijini Dar es Salaam kwa muda wa siku 19.

Akizunghumza na saluti5, Mexime alisema alikuwa bize na mafunzo lakini kwa sasa amemaliza hivyo ameanza kupanga program ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.

“Nataraji kuanza kambi pamoja na mazoezi Julai 17 mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kama unavyotambua Ligi inakuwa na ushindani mkubwa hivyo lazima tujipange vizuri,”alisema.

Akizungumzia kuhusu tetesi za klabu hiyo kumuhitaji mchezaji wa Yanga, Oscar Joshua, alisema hawana mpango wowote wa kuchukua mchezaji huyo kwani tayari walishaweka usajili wao wazi.


Hadi sasa klabu hiyo imefanikiwa kuwasajili wachezaji Juma Nyoso, beki Japhary Kibaya kutoka Mtibwa Sugar, viungo Petter Samson, Mwalyanzi, Ludovic Venancev na mshambuliaji Omary Daga Dagashenko pamoja na kipa Hussein kutoka JKT Ruvu.

No comments