MBAO FC WAVUTA KOCHA MPYA WAKATI ETIENNE NDAYIRAGIJE AKISUASUA KUSAINI KANDARASI MPYA

UONGOZI wa klabu ya Mbao FC Umetafakari kwa muda mrefu kungojea kocha wao mkuu Etienne Ndayiragije kurejea kumwaga wino wa kuendelea kunoa kikosi wakaona isiwe shida wakafanya maaamuzi magumu ya kuvuta kocha mpya Hemed Ally.

Ndauragije anaehusishwa kuchukua mikoba ya kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambuzi mwishoni mwa wiki aliyoonekana viunga vya mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Ally aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja kukinoa kikosi hicho aliiambia saluti5 kuwa amesaini kwa walanda mbao hao kama kocha msaidizi.

“Ni kweli mimi ni mwajiliwa wa Mbao kama kocha msaidizi kuanza msimu ujao ambapo tayari nimeshaanza majukumu yangu na kufanya usajili wa wachezaji kutoka viunga mbalimba vya jiji la Mwanza," alisema.


Hata hivyo mwenyekiti wa klabu hiyo Zephania Njashi alivyopigiwa simu alisema wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumalizana na Ndayiraje kusaini mkataba mpya kwani bado wanahitaji huduma yake kwa hali na mali.

No comments