MBUNGE WA TEMEKE MGENI RASMI UZINDUZI WA FILAMU YA “ASALI WA MOYO”

MBUNGE wa Temeke, Abdallah Mtolea anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio la uzinduzi wa filamu mpya ya Kibongo inayokwenda kwa jina la ‘Asali wa Moyo’, litakalofanyika ndani ya Mpo Afrika Jumapili hii.

Mwandaaji wa muvi hiyo, Profesa Puto ameitonya Saluti5 kuwa, mbali na mbunge Mtolea, amewaalika pia madiwani wa Kata mbalimbali za Wilaya Temeke, wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wadau wa filamu na mashabiki.

“Tumepanga kulifanya tukio hili la uzinduzi kuwa la kihistoria zaidi na tunawaomba wadau na wapenzi wengine wajitokeze kwa wingi kwani hakutakuwa na kiingilio,” amesema Puto ambaye pia ni mwigizaji katika muvi hiyo.

Filamu ya ‘Asali wa Moyo’ inashirikisha mastaa wengi wa muziki na muvi wakiwemo Inspector Haroun, Hamis Korongo, Tausi Ndegela na Vincent Macha.

No comments