MBWEMBWE ZA USHANGILIAJI KAUZU FC NDONDO CUP ZAMDATISHA RAGE

ALIYEKUWA mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amesema kuwa anavutiwa na burudani inayotolewa na timu ya Kauzu FC kwenye michuano ya Ndondo Cup ambayo inaendelea kutimua vumbi katika viwanja tofauti vya jijini Dar es Salaam.

Rage amesema kuwa michuano hiyo inasaidia kupunguza matukio ya uhalifu kwenye kona za jiji la Dar es Salaam.

“Niseme ukweli tu, navutiwa na timu ya Kauzu FC kuanzia namna wanavyoshangilia mpaka wanavyotandaza soka lao, ni kikundi kizuri ambacho hakina vurugu zaidi ya kutoa burudani,” alisema mdau huyo wa soka.

“Uwepo wa michuano hii unasaidia kupunguza matumizi ya mihadarati kwa sababu vijana wengi wanapata kitu mbadala cha kufanya,” aliongeza kiongozi huyo.

“Kuna kila haja ya kuendelea kuisapoti michuano hii kwasababu ni sehemu pekee ambayo vipaji halisi huchomoza, lakini pia kuna burudani ya aina yake kutoka Ndondo Cup na hasa kipindi hiki ambapo Ligi zimemalizika,” alimalizia Rage.


Ismail Aden Rage aliwahi kuwa kiongozi wa Shirikisho la Soka nchini (FAT), kabla ya kuanza kuongoza klabu ya Simba akiwa kama mwenyekiti.

No comments