MDOGO WA ASAMOAH GYAN APIGIWA NDOGONDOGO SIMBA SC

ENDAPO Simba itamalizana vizuri na straika mpya raia wa Ghana, Nicholas Gyan itakuwa imelamba dume kutokana na ubora wa mchezaji huyo.

Taarifa zinasema kuwa, Gyan ambaye ni mdogo wa Asamoah Gyan, nyota na nahodha wa timu ya taifa ya Ghana, ndie mchezaji bora wa Ligi Kuu ya nchi hiyo msimu uliomalizika hivi karibuni ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 19 ambao kwa wachezaji ndio umri wa kuonyesha makali yao.

Taarifa zinadodosa kuwa straika huyo tayari yuko nchini kwa mazungumzo na uongozi na endapo mambo yatakwenda vizuri atamwaga wino Msimbazi.

Kwa mujibu wa mmoja wa watu wa karibu wanaofahamu uwezo wake, wamedai kuwa anajua kufunga kwa staili zote huku pia akiwa na uwezo wa kupiga chenga, kumiliki mpira na kutoa pasi za mabao.


“Tuombe tu wakubaliane na uongozi ili jamaa amwage wino halafu mtauona muziki wake. Na hasa akikutana na watu kama akina Emmanuel Okwi, Laudit Mavugo na John Bocco, kila siku mtakuwa mkisikia timu zimeumia,” alisema mdau huyo aliyejitambulisha kwa jina la Juma Osama.

No comments