MIDDLESBROUGH MBIONI KUMREJESHA VAN PERSIE LIGI YA PREMIER

KAMA mambo yatakwenda kama yalivyopangwa, straika wa zamani wa Arsenal, Robin van Persie atarejea tena kukipiga katika Ligi ya premier.

Mpango huu unafanywa na timu ya Middlesbrough ambao wanapigana vikumbo vya kumwania mpachika mabao huyo.

Taarifa hizi zinanogeshwa na habari za hivi karibuni kutoka nchini Uturuki zinazosema kuwa, klabu anayoichezea ya Fenerbahce imekaribisha ofa kutoka kwa timu zinazomwania straika huyo.

Van Persie alitua kwa vigogo wa soka la Uturuki misimu miwili nyuma akitokea kwa mashetani wekundu wa Manchester United ambapo Middlesbrough wamemtupia ndoano.

Hta hivyo, kinachosubiriwa kwa sasa ni kauli ya kocha wa Fenerbahce, Aitor Karankaambaye ndie atakayeamua kama straika huyo aondoke au la.


Timu hiyo ya England imekuwa na mazungumzo ya mara kwa mara na Mdachi huyo, ikiwa ni pamoja na kufuatilia kiwango chake cha sasa na kujiridhisha kuwa ni kati ya wanandinga watakaoisaidia timu pindi akitua.

No comments